Saturday, April 20, 2013

WAKAWAKA POWER


Watengenezaji wa taa bora ya solar ya Wakawaka, sasa wamekuja na taa nyingine ya solar yenye jina la Wakawaka Power. Tofauti na taa ya mwanzo ya Wakawaka, taa hii ya Wakawaka Power ina uwezo wa kuchaji simu na vifaa vingine vya ki eleketroniki kama Ipad na tablets nyinginezo.

Wakawaka Power inachaji tablet

Viwango vya Wakawaka Power :






  • Betri: 2200 mAh LiPo yenye mizunguko ya kuchaji 1,000. Betri ina uhai wa miaka 5-7.
  • Viunganishi vya USB: USB inayotoa 1A, USB inayoingiza 500 mA
  • Paneli ya solar: Nguvu ya jua uwezo ni 23%, upana na urefu ni 67x100mm. Kiwango cha maisha ya matumizi ni miaka 10 na kuendelea.
  • Menejimenti ya Nishati: Intivation SNBST Toleo la 3.
  • Taa kubwa 2 za LED: Mwanga mkali, Daraja la A, mwanga kwa ujumla ni lumen 60.
  • LED za indiketa: Taa moja nyekundu (inaonyesha kuchaji); Taa 4 za kijani (zinaonyesha ujazo wa betri Taa 1 ya bluu (inaonyesha kuchaji kwa USB)
  • Malighafi: Plastiki rejesho ya ABS
  • Vyeti tha Uthibitisho: CE, inakubalika kwa viwango vya UNFCCC (inasubiri UL)
  • Ukubwa: 120x16x77 mm au 4.7x0.6x3 inchi.
  • Uzito: Karibia gramu 200.
  • Ilivyofungwa: Paketi ya rangi, karatasi ya  FSC, maelekezo ya namna ya kutumia yameambatanishwa.

INAVYOFANYA KAZI
  • Kuchaji: Inajaa kiasi cha 75% kwa masaa 6 (imejaribiwa kwa mwanga wa New York)
  • Kuchaji 100%:  Masaa 4
  • Muda wa kutoa mwanga: 100% kwa masaa 20 na zaidi; 50% masaa 40 na zaidi; 10% masaa 200 na zaidi.
  • Matumizi ya Ziada: Kutuma SOS ukipata dharura (bonyeza kwa sekunde 2); kuhifadhi nguvu ya betri (mwnaga unapungua betri ikianza kwisha); 200% ya mwanga ambao hupungua kuwa 100% baada ya sekunde 30.
kwa maelezo zaidi kuhsu upatikanaji wa Wakawaka Power wasiliana nasi.

                                 
Taa ya Solar ya Wakawaka imefanyiwa majaribio rasmi nchini Tanzania na kuonekana kwamba inafaa sana kwa matumizi yake hasa pale panapo kosekana umeme wa kawaida. Kuwepo kwa mwanga wa jua mkali kwa mwaka mzima kumethibitisha hii taa kuwa bora na yenye manufaa zaidi.


Mlinzi wetu aliipenda Wakawaka kwani ilimpatia mwanga wa kutosha usiku.



Mwanga mwingi wa kutosha unakuwezesha kuchaji Wakawaka mahali popote!