USIKAE GIZANI

Loading...

Wednesday, May 30, 2012

Taa ya Wakawaka Hutumika Popote!

Taa ya Wakawaka inawezwa kutumiwa katika hali zozote zile kuanzia vijijini ambapo hakuna umeme, mijini umeme ukikatika au hata kwenye nyumba za mijini ambapo umeme haujafungwa. Vilevile Wakawaka zinaweza kutumika kama taa ya dharura kwa mfano kwenye gari na sehemu zingine. Hivyo taa hizi zinafaa kwa watu wote ambao wanataka kuwa tayari wakati wowote.

Usisahau kuchukua taa yako ya Wakawaka unaposafiri...itakufaa!

Monday, May 28, 2012

Wakawaka Light: Majaribio ya mwanga wa kusomea


Taa za solar za Wakawaka zinahitajiwa zikidhi mahitaji ya mtumiaji ili aweze kuitumia vizuri. Nimefanya majaribio ya taa hizi na niliona kuwa niliweza kusoma gazeti bila ya shida yeyote.Kama inavyoonekana kwenye hiyo picha hapo juu, ni vizuri kuiweka taa yako katika sehemu iliyo juu ili mwanga ulenge na kumulika moja kwa moja kwenye gazeti au kitabu unachokisoma. Kama mwanga unaohitajika ni wa kumulika chumba kizima, taa hiyo inawezwa kutundikwa kutoka juu ya dari, hivyo kukiangaza chumba kizima. (angalia picha hiyo hapo chini).Taa hiyo inatoa mwanga mzuri mkali unaotoa mandhari ya kupendeza.Baada ya kufanyika kwa majaribio haya, taa hizi zitapelekwa vijijini (na pia hata vile mijini) kwa majaribio zaidi na kupata mawazo ya watumiaji kuhusu ubora wa taa na mawaidha ya kuziboresha zaidi.

Blog ya Wavuti yahimiza Nishati Endelevu
Blog ya Wavuti imeungana nasi katika kueneza habari kuhusu matumizi ya vibatari na athari zake. Kwa kufanya hivyo inasaidia katika kubadilisha fikra za watu kutoka kujiona na kutokuwa na uwezo wa kugeuza na kuendeleza maisha yao, hadi kufikia hatua ya kubadilisha maisha yao wenyewe. Habari hizo zinapatikana hapa:

http://www.wavuti.com/4/post/2012/05/kibatari.html#axzz1w9LYryy7

Saturday, May 26, 2012

Majaribio ya Taa ya Wakawaka

 

Nimepokea taa za Wakawaka kutoka Uholanzi na zimefanyia majaribio. Nimeridhishwa sana na utendaji wa taa hizi kwa vile zinafanya vile kama ilivyoelezwa kwenye tovuti ya wavumbuzi wa taa hii www.wakawakalight.com

Baada ya kuchaji taa kwenye jua kwa masaa kama 8 hivi niliiwasha kuanzia majira ya saa nne za usiku. Taa hii iliwaka kwa mwanga uleule na kuanza hadi asubuhi saa tatu. Mwanga ulianza kufifia kama saa tano asubuhi, lakini iliendelea kuwaka. Hii inathibitisha kuwa taa hii hutoa mwanga muda mrefu sana tofauti na taa zingine za solar.

Taa ya solar ya Wakawaka ikiwa imetundikwa

Taa ya solar ya Wakawaka kutoka kwenye kasha lake
Watu wengi wanatumia mwanga wa kibatari pale ambapo hakuna umeme. Pamoja na kutoa mwanga hafifu, kibatari kinatoa moshi mwingi mweusi ambao ni hatari kwa mtumiaji akipumua moshi wake. Kibatari hutumia mafuta ya taa ambayo ni ghali sana na hivyo kupunguza kipato na kuchangia katika kuleta umasikini. Taa ya solar ya Wakawaka ina mwanga mkali, usio na moshi na hutumia betri ambazo ni rahisi na zinazohitaji kubadilishwa baada ya miaka mitatu.


Kuelezea kuhusu matumizi na faida za taa ya solar ya Wakawaka
Saturday, May 12, 2012

Taa ya Wakawaka Tanzania


Kwa vile uvumbuzi uliotumiwa katika taa hizi ni mpya kabisa, ndio kwanza taa za kwanza zimetoka kiwandani mwezi huu wa Mei 2012. Tunatarajia kuzipeleka kwa wananchi, hasa wale waishio vijijini na kutaka kuona mawazo yao kwanza kuhusu taa hizi. Baada ya taa hizi kutengenezwa, zilifanyiwa majaribio na zimedhihirika kuwa zinaweza kukabili mazingira magumu sana, kama vile kunyeshewa na mvua, kuzamishwa kwenye maji na hata kuvumilia joto kali.


Habari zaidi utazipata www.bestlifeafrica.org


Wednesday, May 9, 2012

Usikae gizani, tumia taa ya Solar ya Wakawaka
Tatizo la kukosekana kwa nishati ya umeme mijini na vijijini limekuwa sugu sasa. Hata hivyo nchi ya Tanzania na Africa nzima kwa ujumla imebahatika kuwa na mwanga mwingi wa jua. Jua linawaka mchana na hutupa mwanga wakati huo. Je unajua kwamba tunaweza kutumia jua hilo usiku pia? Ndio tunaweza, kwa kutumia taa za solar. Faida za kutumia taa za solar ni kama zifuatazo:
 • Hukutoa katika umasikini, 
 • Unakuwa na afya nzuri kwa kupumua hewa safi,
 • Wanafunzi hupata matokeo mazuri shuleni, 
 • Na mengineyo mengi...

Taa za solar nini?

Taa za solar ni taa ambazo zinatumia mionzi ya jua ambapo mionzi hiyo hugeuzwa na kuwa umeme ambao huhifadhiwa katika betri. Betri hizo hutumika pamoja na balbu kutupatia umeme na kupata mwanga. Kwa kutumia taa za solar utaepukana na gharama za mafuta ya taa na pia kuepusha hatari ya vifo vitokananvyo na kuungua kwa ajali za moto.
BestLife Africa pamoja na Off-Grid Solutions wanaleta Tanzania kwa mara ya kwanza taa ya solar ya WakawakaWakawaka ni taa ambayo inatofautiana sana kiubora na taa zingine za solar. Tofauti zake ni:

Mwanga 
 • Inatoa mwanga mkali sana kwa masaa 8.
 • Inakupa masaa 16 ya mwanga wa kujisomea.
 • Inakupa masaa 80 ya mwanga wa ulinzi wa usiku kwa kuchaji mara moja (kwa siku).


Kuchaji

Kutokana na utaalamu wa hali ya juu wenye hati miliki wa kampuni ya Kiholanzi, Intivation, unaweza kuchaji taa hiyo kwa namna zifuatazo:

 • Inaweza kuchaji zaidi ya mara mbili katika hali ambayo hakuna mwanga mzuri.
 • Inaweza kuchaji hata kwa kutumia mwanga ambao si wa jua.Umbo

 • Ni rahisi kuishika.
 • Inabebeka mahali popote
 • Unaweza kuitundika
 • Inakaa kwenye chupa
 • Ina umbo zuri na la kupendeza

Betri
 • Inatumia betri ya LiFePo4 
 • Unaweza kuitumia betri hiyo kwa muda wa miaka mitatu
 • Huhimili hali ya joto kali
      
   
  *Uwezo wa kuchaji betri za simu (Hii inafanyiwa matengenezo bado)

  Shida kubwa nyingine ambayo inatokana na kukosekana kwa umeme ni kutoweza kuchaji betri ya simu yako. Kwa kutumia taa ya Wakawaka, licha ya kupata mwanga usiku, unaweza vilevile kuchaji betri yako ya simu.   Kwa maelezo zaidi kuhusu taa hizi za Wakawaka wasiliana nasi kwa kututumia barua pepe info@bestlifeafrica.org