Wednesday, May 9, 2012

Usikae gizani, tumia taa ya Solar ya Wakawaka




Tatizo la kukosekana kwa nishati ya umeme mijini na vijijini limekuwa sugu sasa. Hata hivyo nchi ya Tanzania na Africa nzima kwa ujumla imebahatika kuwa na mwanga mwingi wa jua. Jua linawaka mchana na hutupa mwanga wakati huo. Je unajua kwamba tunaweza kutumia jua hilo usiku pia? Ndio tunaweza, kwa kutumia taa za solar. Faida za kutumia taa za solar ni kama zifuatazo:
  • Hukutoa katika umasikini, 
  • Unakuwa na afya nzuri kwa kupumua hewa safi,
  • Wanafunzi hupata matokeo mazuri shuleni, 
  • Na mengineyo mengi...

Taa za solar nini?

Taa za solar ni taa ambazo zinatumia mionzi ya jua ambapo mionzi hiyo hugeuzwa na kuwa umeme ambao huhifadhiwa katika betri. Betri hizo hutumika pamoja na balbu kutupatia umeme na kupata mwanga. Kwa kutumia taa za solar utaepukana na gharama za mafuta ya taa na pia kuepusha hatari ya vifo vitokananvyo na kuungua kwa ajali za moto.




BestLife Africa pamoja na Off-Grid Solutions wanaleta Tanzania kwa mara ya kwanza taa ya solar ya WakawakaWakawaka ni taa ambayo inatofautiana sana kiubora na taa zingine za solar. Tofauti zake ni:





Mwanga 
  • Inatoa mwanga mkali sana kwa masaa 8.
  • Inakupa masaa 16 ya mwanga wa kujisomea.
  • Inakupa masaa 80 ya mwanga wa ulinzi wa usiku kwa kuchaji mara moja (kwa siku).






Kuchaji

Kutokana na utaalamu wa hali ya juu wenye hati miliki wa kampuni ya Kiholanzi, Intivation, unaweza kuchaji taa hiyo kwa namna zifuatazo:

  • Inaweza kuchaji zaidi ya mara mbili katika hali ambayo hakuna mwanga mzuri.
  • Inaweza kuchaji hata kwa kutumia mwanga ambao si wa jua.







Umbo

  • Ni rahisi kuishika.
  • Inabebeka mahali popote
  • Unaweza kuitundika
  • Inakaa kwenye chupa
  • Ina umbo zuri na la kupendeza

Betri
  • Inatumia betri ya LiFePo4 
  • Unaweza kuitumia betri hiyo kwa muda wa miaka mitatu
  • Huhimili hali ya joto kali
        
     
    *Uwezo wa kuchaji betri za simu (Hii inafanyiwa matengenezo bado)

    Shida kubwa nyingine ambayo inatokana na kukosekana kwa umeme ni kutoweza kuchaji betri ya simu yako. Kwa kutumia taa ya Wakawaka, licha ya kupata mwanga usiku, unaweza vilevile kuchaji betri yako ya simu. 



    Kwa maelezo zaidi kuhusu taa hizi za Wakawaka wasiliana nasi kwa kututumia barua pepe info@bestlifeafrica.org

No comments:

Post a Comment