Saturday, May 26, 2012

Majaribio ya Taa ya Wakawaka

 

Nimepokea taa za Wakawaka kutoka Uholanzi na zimefanyia majaribio. Nimeridhishwa sana na utendaji wa taa hizi kwa vile zinafanya vile kama ilivyoelezwa kwenye tovuti ya wavumbuzi wa taa hii www.wakawakalight.com

Baada ya kuchaji taa kwenye jua kwa masaa kama 8 hivi niliiwasha kuanzia majira ya saa nne za usiku. Taa hii iliwaka kwa mwanga uleule na kuanza hadi asubuhi saa tatu. Mwanga ulianza kufifia kama saa tano asubuhi, lakini iliendelea kuwaka. Hii inathibitisha kuwa taa hii hutoa mwanga muda mrefu sana tofauti na taa zingine za solar.

Taa ya solar ya Wakawaka ikiwa imetundikwa

Taa ya solar ya Wakawaka kutoka kwenye kasha lake




Watu wengi wanatumia mwanga wa kibatari pale ambapo hakuna umeme. Pamoja na kutoa mwanga hafifu, kibatari kinatoa moshi mwingi mweusi ambao ni hatari kwa mtumiaji akipumua moshi wake. Kibatari hutumia mafuta ya taa ambayo ni ghali sana na hivyo kupunguza kipato na kuchangia katika kuleta umasikini. Taa ya solar ya Wakawaka ina mwanga mkali, usio na moshi na hutumia betri ambazo ni rahisi na zinazohitaji kubadilishwa baada ya miaka mitatu.


Kuelezea kuhusu matumizi na faida za taa ya solar ya Wakawaka




No comments:

Post a Comment